Kocha mpya wa Azam FC, Mzambia George Lwandamina, ameanza rasmi kazi ya kukinoa kikosi cha timu hiyo leo Alhamisi, ikiwa ni mara yake ya kwanza tangu ajiunge rasmi na vijana hao wa Chamazi mapema wiki iliyopita.
Lwandamina ana kazi kubwa ya kufanya kukiweka sawa kikosi hicho kilichokosa mwelekeo baada ya kupoteza uongozi wa ligi ikizidiwa alama saba na vinara Yanga sc huku wakiwa wamecheza michezo sawa 14.