Siku ya kesho Jumamosi mabondia 20 watazichapa katika pambano la kuwapata mabondia nane watakaoiwakilisha Mwanza kwenye mashindano ya ngumi za ridhaa Taifa tarehe 25 March mkoani Tanga.
Jopo la makocha wamejiandaa vyema kuchagua mabondia wazuri watakaowachuja na kuwaingiza kambini kwa ajili ya kujiandaa na mashindano hayo ya kuuwakilisha mkoa wa Mwanza.
Katibu wa chama cha ngumi za ridhaa wilaya ya Nyamagana ,Hamad Mabula amesema kuwa pambano hilo litafanyika ukumbi wa Bundasliga uliopo eneo la Nyasaka na mabondia wote wameshakamilisha kupima uzito pamoja na afya zao tayari kabisa kwa pambano hilo.