Nyota anayekipiga ndani ya klabu ya AC Milan,Zlatan Ibrahimovic amewekwa kwenye rada za Hammarby ya nchini Sweden ambayo inataka saini yake pindi akimalizana na timu yake ya sasa.
Mkataba wa Zlatan na mabosi wake wa AC Milan unakaribia kuisha mwishoni mwa msimu huu kwani alisaini kandarasi ya miezi sita pekee jambo linalowapa matumaini mabosi hao wa Hammarby.
Zlatan raia wa Sweden amecheza mechi 10 na kutupia mabao manne pia hapo awali aliwahi kukipiga ndani ya Barcelona, Manchester United, Ajax, PSG na LA Galaxy.