Home Makala Mabosi Yanga Sc Wamalizana na Pacome,Maxi

Mabosi Yanga Sc Wamalizana na Pacome,Maxi

Majeruhi Yamweka Matatani Yao Kouasi

by Sports Leo
0 comments

Mabosi wa klabu ya Yanga sc wamefanya haraka kumaliza mazungumzo ya kuongeza mikataba mipya kwa mastaa wake wawili Pacome Zouzoua na Maxi Nzengeli ambao mikataba yao inaelekea ukingoni mwishoni mwa msimu huu.

Mastaa hao walikua na mikataba ya miaka miwili walipojiunga na kikosi hicho msimu 2023-2024 ambapo Maxi alisajiliwa akitokea Maniema Union ya Dr Congo huku Pacome Zouzoua akitokea nchini kwao Ivory coast.

Kutokana na viwango vyao vya hali ya juu mastaa hao walikua na ofa kutoka vilabu mbalimbali nchini na nje ya nchi ambapo vilabu vya Simba sc na Azam Fc walikua wakiwafukuzia kwa ukaribu.

banner

Taarifa njema kwa wananchi ni kwamba mastaa hao tayari wamekamilisha mazungumzo ya kuongeza mikataba mipya ambayo wataisaini hivi karibuni  baada ya kukubaliana kuhusu mshahara na pesa ya usajili kwa mikataba ya miaka miwili kwa kila mmoja.

Hata hivyo kwa upande wa beki Yao Kouassi bado mabosi wa klabu hiyo wanaangalia mstakabali wa majeraha yanayomkabili kabla ya kufanya uamuzi kuhusu kumsainisha mkataba mpya wa miaka miwili.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited