Home Makala Man City Yaikalisha Real Madrid

Man City Yaikalisha Real Madrid

by Sports Leo
0 comments

Klabu ya Manchester City imeibuka na ushindi wa mabao 4-3 dhidi ya Real Madrid mchezo wa nusu fainali ya Uefa Champions League mchezo uliofanyika katika uwanja wa Ettihad jijini Manchester.

Iliwachukua Manchester City dakika mbili tu kupata uongozi wa mchezo kwa bao la Kevin De Bryne na kisha baadae Gabrier Jesus kufunga bao la pili dakika ya 11 lakini Karim Benzema akasawazisha dakika ya 32  akiunganisha krosi ya Mendy na kufanya mchezo kwenda mapumziko matokeo yakiwa 2-1.

Phil Foden alifunga bao dakika ya 52 lakini bao hilo lilidumu dakika 2 tu baada ya ViniciusJr kusawazisha bao hilo na kufanya mchezo usomeke 3-2 wenyeji wakiongoza na baadae walifanikiwa kupata bao dakika ya kupata bao la nne likifungwa na Bernado Silva dakika 74 lakini Karim Benzema alifunga bao la tatu dakika 82 na kufanya mchezo kumalizika kwa 4-3 na kusubiri mchezo wa marudiano wiki ijayo Santiago Bernabeu.

banner

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited