Kipa wa klabu ya Simba Sc Aishi Manula amekua ni miongoni mwa magolikipa wa klabu hiyo waliosafiri na msafara wa timu hiyo kuelekea Visiwani Zanzibar kwa ajili ya mechi ya fainali ya michuano ya kombe la Shirikisho barani Afrika dhidi ya Rs Berkane.
Mara nyingi msimu huu klabu hiyo imekua nadra kusafiri na kipa huyo ambapo mara nyingi husafiri na kipa Moussa Camara na Hussein Abel sambamba na Ally Salim.
Manula alipoteza namba klabuni hapo baada ya kuruhusu mabao matano katika ushindi wa 5-1 walioupata Yanga sc katika mchezo dhidi ya Klabu hiyo.
Tangu hapo klabu hiyo ilimsajili Moussa Camara ambaye amekua na kiwango bora na kuwasahaulisha mashabiki kuhusu Manula na ambapo mara chache anapokosekana basi Ally Salim amekua akiziba pengo hilo.
Msafara wa klabu hiyo upo Visiwani Zanzibar kwa ajili ya maandalizi ya mwisho kuelekea mchezo wa pili wa fainali dhidi ya Rs Berkane utakaofanyika katika uwanja wa New Amaan complex siku ya Jumapili Mei 25 2025 ambapo katika mchezo wa awali Simba sc walikubali kipigo cha mabao 2-0.