Home Makala Mashaka Atambulishwa Simba Sc

Mashaka Atambulishwa Simba Sc

by Sports Leo
0 comments

Klabu ya Simba imekamilisha uhamisho wa mshambuliaji Valentino Mashaka kutoka klabu ya Geita Gold kwa mkataba wa miaka miwili na ametangazwa rasmi hii leo kuwa mchezaji wa klabu hiyo.

Valentino Mashaka Kusengama msimu uliopita amefunga magoli sita [6] na kutoa pasi moja [1] ya goli na kumfanya kuwa mfungaji bora wa kikosi cha Geita Gold Fc ambacho kimeshuka daraja msimu huu wa ligi kuu.

Mashaka anakuja kwa ajili ya kurudisha furaha kwa wanasimba ambao wameikosa kwa miaka takribani mitatu baada ya kukosa makombe yote muhimu kwa misimu yote mitatu wakiacha utawala kwenda kwa Yanga sc.

banner

Usajili wa mshambuliaji huyo unakwenda kuungana na mastaa wazawa kama Kibu Dennis katika eneo la ushambuliaji ili kuleta furaha kwa mashabiki wakiungana na usajili mpya kama Steven Mukwala,Fredy Michael na Pa Omar Jobe ambao tayari wameshazoea mazingira ya klabu hiyo.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited