Mshambuliaji Fiston Mayele ameibuka mshindi wa tuzo ya mfungaji bora wa michuano ya klabu bingwa barani Afrika (Cafcl) baada ya kufunga mabao sita akiwaacha Emam Ashour wa Al Ahly na Ibrahim Adel wa Pyramids wenye mabao matano kila mmoja.
Fiston Mayele amewapiku wenzake baada ya kufunga bao la utangulizi kwa Pyramids kwenye mchezo wa Fainali uliofanyika usiku ya juni mosi 2025.
Pyramids Fc wamecheza fainali yao ya pili ya michuano ya CAfcl na kati ya hizo walipoteza moja ya kombe la Shirikisho dhidi ya RS Berkane msimu wa mwaka 2019/20 kabla ya kucheza Cafcl dhidi ya Mamelodi Sundowns na kushinda rasmi ubingwa wao wa kwanza wa CAF.
Pyramids ndani ya Kundi D msimu huu walimaliza wakiwa na alama 13 sawa na Esperance de Tunis lakini idadi ya mabao ndio iliwatofautisha kwenye nafasi zao, huku Robo Fainali wakiitoa FAR Rabat kisha Orlando Pirates ndani ya Nusu Fainali na Fainali wameshinda mbele ya Masandawana.