Home Soka Mayele Kutimka Yanga sc

Mayele Kutimka Yanga sc

by Sports Leo
0 comments

Mabosi wa klabu ya Yanga sc wanakuna kichwa kufuatia mshambuliaji Fiston Mayele kupokea ofa ya mshahara mnono kutoka klabu ya Rs Berkane inayonolewa na kocha mkongo Florent Ibenge ambaye amevutiwa na kiwango cha staa huyo.

Mayele ambaye msimu huu amekua wa moto akifunga mabao 14 ya ligi kuu nchini huku pia akiwa na asisti tatu amemvutia kocha wa klabu hiyo iliyoko nchini Moroco ambao ni mabingwa wa kombe la shirikisho ambao wanataka kuununua mkataba wake wa mwaka mmoja uliosalia katika klabu ya Yanga sc.

Inasemekana mshambuliaji huyo hana shida na suala la kuhama endapo mabosi wa klabu ya Yanga sc watamuongezea mshahara pamoja na marupurupu ili asaini mkataba wa mwaka mmoja zaidi kusalia jangwani ili akae hapo kwa miaka miwili tofauti na mmoja uliopo sasa.

banner

Mayele alijiunga na Yanga sc msimu uliopita akitokea klabu ya As Vita ambapo alisajiliwa na Yanga sc kama mchezaji huru baada ya kumaliza mkataba klabuni As Vita na sasa amekua lulu hapa nchini hasa kutokana na staili yake ya kushangilia ya kutetema.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited