Leo ligi kuu Tanzania bara itaendelea kuchanja mbunga kwa timu 16 kuwa uwanjani kuzisaka pointi tatu muhimu katika viwanja tofauti.
Ratiba ya mechi zitakazocheza saa 10:00 jioni ni ;Singida v Polisi Tanzania, Namfua.Kagera Sugar v Prisons, Kaitaba.Ruvu v Mbao, Mabatini.Biashara v Mbeya City, Karume.Mtibwa v Ndanda, Gairo na JKT Tanzania v Azam katika uwanja wa Jamhuri.
Yanga Sc v Alliance ni mechi itakayopigwa saa 1:00 usiku katika uwanja wa Taifa jijini Dar-es -salaam.