Kocha mkuu wa klabu ya Yanga sc Miloud Hamdi amechaguliwa kuwa kocha bora wa mwezi April wa ligi kuu ya Nbc nchini baada ya kupata matokeo bora zaidi kuzidi wapinzani wake katika michezo ya ligi kuu kwa mwezi huo.
Miloud amewashinda Aman Josiah wa Tanzania Prison na David Ouma wa Singida Black Stars ambao aliingia nao fainali katika tuzo hiyo.
Miloud aliyejiunga na Yanga sc akitokea Singida Black Stars aliingoza Yanga sc katika michezo minne iliyocheza mwezi huo akizifunga klabu za Tabora United 3-0,Coastal Union 1-0,Azam Fc 2-1 na Fountain Gate Fc 4-0.

🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Pia Kiungo wa ushambuliaji wa klabu ya Dodoma Jiji Fc Iddy kipagwile ameshinda tuzo hiyo ya mchezaji bora wa mweziAprili huku akiwashinda Haruna Chanongo wa Tanzania Prison na Pacome Zouzoua wa Yanga sc.
Kipagwile katika michezo minne ya klabu hiyo alifunga mabao matatu na kutoa asisti tatu zilizomfanya kutwaa tuzo hiyo.
