Home Soka Mnigeria Njiani Kutua Simba Sc

Mnigeria Njiani Kutua Simba Sc

by Sports Leo
0 comments

Nyota wa Klabu ya Rivers United Augustine Okejepha yupo njiani kuja Tanzania kwa ajili ya kujiunga na mabingwa wa zamani wa Ligi kuu Tanzania Bara klabu ya Simba baada ya kufikia makubaliano baada ya mazungumzo ya muda mrefu.

Kiungo huyo wa ulinzi punde tu baada ya kutua nchini muda wowote atatangazwa rasmi na klabu hiyo kama mchezaji mpya huku akisifika kutokana na uwezo wake  mkubwa sana wa kufunga magoli licha ya kuwa ni kiungo.

Mchezaji huyo wa zamani wa Kano Pillars ya nchini Nigeria anasifika zaidi kwa umahiri wake wa kucheza vizuri zaidi kiungo cha chini na juu kwa ufasaha huku akiwa na uwezo mkubwa wa kufunga magoli kitu kinachompa faida ya ziada kuanza kikosini.

banner

Usajili wa mchezaji huyo unamaanisha kuwa Simba Sc inaweza kuachana na Babacar Sarr muda wowote kutokana na kupata mbadala wake ambaye atacheza na Donald Ngoma katika eneo la kiungo cha chini huku pia Sadio Kanoute nae anaweza kumpisha staa huyo hasa baada ya kusemekana kuwa ameomba yeye mwenye kuondoka klabuni hapo.

 

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited