Staika wa mabao kwenye klabu ya Yanga , DavidMolinga ‘Falcao’ amepokea barua inayompa siku tatu za kujieleza kwa nini asichukuliwe hatua za kinidhamu.
Uongozi huo umetoa barua hiyo baada ya kupokea sare na Namungo huko mkoani Lindi ambayo inawafanya wawe na sare tisa msimu huu wa ligi kuu .
Katika maelezo ya barua hiyoMolinga atapewa adhabu kali endapo atashindwa kutoa maelezo yenye mashiko ndani ya siku hizo ili iwe fundisho kwa wachezaji wengine wa klabu hiyo.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Kocha mkuu wa Yanga, Luc Eymael ameonekana kukerwa na tabia ya baadhi ya wachezaji wa Yanga kwani kabla ya mchezo wa Namungo alibainisha wachezaji wake wanachagua mechi wakitaka wapangwe zile kubwa.