Safari ya michuano ya Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ndani iliyofanyika katika nchi tatu kwa pamoja za Afrika mashariki za Tanzania,Kenya na Uganda (Chan Pamoja) imemalizika kwa ushindi wenye msisimko na historia ikiwa imeandikwa tena ambapo Morocco wamefunga ukurasa wa ushindi katika fainali hizo kwa mwaka 2024, baada ya kuwafungia Madagascar mabao 3-2 na kushinda taji lao la tatu.
Ushindi huu unafanya Morocco kuwa timu yenye mafanikio makubwa zaidi katika historia ya mashindano haya ambayo yamefanyika kwa mara ya kwanza katika nchi hizo tatu za Afrika Mashariki licha ya wenyeji wote watatu kutolewa katika hatua ya robo fainali licha ya kuwa na hamasa ya mashabiki wa nyumbani wa kutosha ambapo Morocco ambao ni mabingwa waliwatoa Tanzania kwa kuwafunga 1-0.
Oussama Lamlioui Aweka Historia Tena
Pamoja na kufunga bao pekee la kuwatoa wenyeji Tanzania katika uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam,Hakuishia hapo kwani Katika fainali iliyojaa msisimko, Oussama Lamlioui, mshambulizi wa Morocco, alikuwa nyota wa mechi hiyo akifunga mara mbili na kumaliza kama mfungaji bora wa mashindano hayo baada ya kufikisha mabao sita.
Lakini kile kinachogonga vichwa vingi vya habari, ni goli lake la mwisho la kupindua mechi ambalo alifunga kwa mkwaju wa mbali kabisa, karibu mita 40, kama mfano wa ubunifu ukijumlisha na nguvu na silaha ya kufanya maamuzi magumu ambapoa alipiga shuti kali takribani mita arobaini na kujaa moja kwa moja wavuni na kuwaacha Madagascar wakiwa hawana la kufanya.
Fainali Yenye Ushindani Mkali
Madagascar waliweka Morocco chini ya shinikizo kwa kufunga kwanza kupitia Clavin Felicite ‘Fely’ Manohantsoa kwa mkwaju mzuri dakika ya 9 ya mchezo lakini Morocco wakajipata kwenye mchezo tena kupitia Youssef Mehri, aliyefanikiwa kuirejesha timu mchezoni dakika ya 27 kwa kumalizia kwa kichwa krosi ambayo mabeki wa Madagascar walichelewa kuokoa.
Oussama Lamlioui akachangia tena kwa kuwaongoza kwa bao la pili kabla ya mapumziko, na kuongeza msisimko mkubwa kwa mashabiki waliojaa katika uwanja huo wa Moi Kasarani jijini Nairobi lakini Madagascar hawakuridhika ambapo juhudi na maarifa ya Toky Niaina Rakotondraibe yalisababisha alisawazisha dakika ya 68, akifungua mbio za kusawazisha tena.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Hata hivyo tena,Mwisho ulipambwa tena na goli la mwisho la zuri alilofunga staa Lamlioui na hatimaye kuwa shujaa kamili wa Morocco katika fainali hizo ambapo staa huyo wa Rs Berkane ameonyesha kuwa ni aina ya mshambuliaji ambaye anahitaji nafasi moja pekee kumaliza mchezo.
Muendelezo wa Utawala Morocco
Tangu fainali zilizoanza mwaka 2009, Morocco sasa wamekamilisha historia kwa kuwa timu ya kwanza kushinda CHAN mara tatu, wakishinda taji la 2018, 2020, na sasa 2024 ambapo mpaka sasa silaha yao kubwa ni kuwa na wachezaji wa ndani wanaocheza klabu zao za nyumbani kubwa za Wydad Athletic Club,Raja Athletic club na Rs Berkane ambazo pia zinafanya vizuri katika michuano ya ngazi ya vilabu barani Afrika.
Mwisho wa Fainali za Kihistoria Afrika Mashariki
Fainali hii iliyopita ilikuwa mwisho wa mashindano ya mwezi mzima yaliyoandaliwa kwa pamoja na Kenya, Tanzania na Uganda ambapo imekua ni mara ya kwanza CHAN ikishirikishwa na nchi tatu kwa ujumla wake huku michuano hiyo ikitumika kama sehemu ya maandalizi kueleka michuano mikubwa ya mataifa ya Afrika ambayo pia itafanyika katika nchi hizo tatu kwa pamoja ambapo sasa waandaaji ambao ni Shirikisho la soka barani Afrika (Caf) watakua wamejua wapi panapovuja.