Site icon Sports Leo

Morrison Apaa Kuifuata Kaizer Chiefs

Mshambuliaji wa klabu ya Simba sc Benard Morrison ameungana na timu hiyo nchini Afrika ya kusini baada ya kufanikiwa kusafiri leo kuelekea mchezo wa timu hiyo dhidi ya Kaizer Chiefs utakaofanyika siku ya Jumamosi.

Awali kikosi cha timu hiyo kilisafiri jana kuelekea nchini humo ambapo staa huyo hakusafiri kutokana na sababu zilizoelezwa na meneja wa klabu hiyo Rweyemamu kuwa ni sababu binafsi.

Lakini hivi leo mchezaji huyo ameposti picha katika mitandao yake ya kijamii akiwa uwanja wa ndege akielekea nchini humo.

Exit mobile version