Bernard Morrison kiungo mshambuliaji wa Yanga amesema kuwa kwa kipindi hiki cha maambukizi ya Corona anachukua tahadhari kwa kukaa ndani na kusikiliza muziki ili kuwa salama.
” Ninachokifanya kwa sasa ni kuchukua tahadhari ambapo najiepusha na mikusanyiko ya watu pamoja na kujichanganya sehemu ambazo sio salama kwa lengo la kujikinga”
“Napenda kusikiliza muziki na kufanya mazoezi binafsi ili kulinda kipaji changu, kikubwa ni kuona kwamba kunakuwa na hali ya utulivu na ile hofu inaondoka”alisema Morrison
Ligi Kuu Bara imesimamishwa na Serikali, Machi 17 na inatarajiwa kurejea baada ya mwezi mmoja iwapo hali ya maambukizi ya Virusi vya Corona yatapungua.