Kocha mkuu wa Tottenham,Jose Mourinho ametoa msaada wa chakula kwa wazee wa kituo cha Your Door Step kilichopo Enfield.
Mourinho aliwatembelea watu wa kituo hicho kilicho karibu na sehemu ya kufanyia mazoezi ya timu yake ya Spurs ambapo aliwapelekea chakula na vitu muhimu ikiwa ni sehemu ya msaada kwa jamii inayomzunguka.
Wazee hao walishauriwa kukaa karantini kwa muda wa wiki 12 ili kujikinga na maambukizi ya Virusi vya Corona ambayo kwa sasa yameshaenea takribani dunia nzima.
“Nipo hapa kwenye kituo cha Love Your Door Step Enfield kwa ajili ya kuchangia kile ambacho ninacho ambacho ni chakula na unaweza kujitoa pia kwa ajili ya kuwapa msaada iwe ni chakula, fedha ama kujitoa kwa ajili yao,” amesema kupitia video iliyotumwa na Love Your DoorStep kwenye akaunti ya Twitter.