Home Soka Mpanzu Atua Simba Sc

Mpanzu Atua Simba Sc

by Sports Leo
0 comments

Klabu ya Simba Sc iko mbioni kukamilisha usajili wa mchezaji Ellie Mpanzu kutoka klabu ya As Vita ya nchini Congo Dr baada ya kufikia makubaliano ya maslahi binafsi na mchezaji huyo ambaye muda wowote anaweza kutua hapa nchini kwa ajili ya kukamilisha taratibu za mwisho za usajili.

Mpanzu mwenye miaka 22 yupo katika orodha ya wachezaji wanaowindwa na Simba sc tangu mwanzoni mwa msimu huu wakati wa usajili wa dirisha kubwa lakini dili hilo halikufanikiwa na badala yake akasajiliwa Willy Esomba Onana ambaye ameshindwa kukidhi matarajio.

Mpanzu amemaliza msimu akiwa na mabao 11 akicheza zaidi kama winga wa kulia ama kushoto huku pia akiwa na uwezo mzuri wa kucheza kama mshambuliaji namba mbili.

banner

Msimu huu Simba sc imepanga kufanya maboresho makubwa ya kikosi chake kwa kusajili majembe ya maana huku ikilenga zaidi kusajili vijana ambao watadumu kikosini humo kwa miaka kadhaa ili kurejesha heshima yao iliyopotea baada ya kukosa makombe kwa msimu wa tatu mfululizo sasa.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited