Home Soka Mpanzu,Simba Sc Mambo Safi

Mpanzu,Simba Sc Mambo Safi

by Sports Leo
0 comments

Klabu ya Simba Sc imekamilisha usajili wa mshambuliaji raia wa Congo Drc Ellie Mpanzu kwa mkataba wa miaka mitatu akiwa kama mchezaji huru baada ya kumalizana na klabu yake ya As Vita.

Mpanzu mpaka sasa yupo nchini akiwa amemalizana na Klabu hiyo na anatarajiwa kuwepo siku ya Jumapili kuiona Simba sc ikivaana na Al ahly Tripol katika mchezo wa marudiano wa hatua ya pili ya michuano ya kombe la Shirikisho barani Afrika.

Simba sc imemwambia Mpanzu ajiunge na kambi ya timu hiyo mapema ili azoee mazingira na ataanza kutumika mwezi Januari wakati usajili wa dirisha dogo utakapofunguliwa.

banner

Mpanzu amerudi kukubaliana na Simba sc baada ya dili lake la kutimkia barani ulaya kushindikana baada ya kutofanikiwa katika majaribio yake ya kujiunga na klabu ya Krc Genk ya nchini Ubelgiji.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited