Home Makala Mrithi wa Yao Kuwasili Jangwani

Mrithi wa Yao Kuwasili Jangwani

by Sports Leo
0 comments

Klabu ya Yanga sc ipo mbioni kumleta nchini beki wa klabu ya Tp  Mazembe Ibrahim Keita kwa ajili ya kufanya mazungumzo na mabosi wa timu hiyo inayompigia hesabu kumsajili kwa kikosi cha msimu ujao.

Mabosi wa Yanga wameona ni vyema kumuita beki huyo Dar ili kufanya mazungumzo ya mwisho kabla ya kumpa mkataba katika kikosi hicho, ikielezwa ataziba pengo la Yao Kouassi ambaye kwa sasa ni majeruhi na mmoja ya wachezaji waliokosekana uwanjani kwa muda mrefu.

banner

Keita ambaye ameichezea Mazembe ndani ya misimu mitatu, mkataba wake kwa sasa upo ukingoni na klabu ya hiyo huku kukiwa hakuna makubaliano rasmi yaliyofikiwa kuhusu kuongeza mkataba klabuni hapo.

“Makubaliano yao ni kuja huko Juni 12 ili kuonana na mabosi wa Yanga kwa ajili ya kukamilisha mazungumzo yao na inavyoonekana kila kitu kiko vyema,” alisema mtu huyo wa karibu na beki huyo alipoulizwa na mwandishi wetu kuhusu tetesi usajili huo.

Hata hivyo pia mchezaji huyo naye alikiri kufanya mazungumzo na klabu hiyo ambayo mpaka sasa yanaelekea pazuri.

“Ni kweli nimefanya mazungumzo na Yanga, lakini bado hatujafikia makubaliano, nilikiona kikosi chao katika michuano ya kimataifa, ni timu nzuri”,Alisema na kuendelea kuwa

“Kwa sasa namalizia mkataba wangu, lakini misimu mitatu ni mingi kucheza timu moja, mipango yangu ni kutafuta changamoto mmpya.alimalizia kusema beki huyo mwenye rasta.

Yanga sc wanataka kumsajili beki huyo kuziba pengo la Yao Kouassi ambaye ana majeraha ya muda mrefu na hivi karibuni alifanyiwa upasuaji wa goti jambo ambalo litamuweka nje mpaka mwanzoni ama katikati ya msimu ujao ambapo ndipo atakua fiti kwa asilimia mia.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited