Home Soka Msauzi Anukia Simba Sc

Msauzi Anukia Simba Sc

by Sports Leo
0 comments

Klabu ya Simba sc inafikiria kumuajiri kocha wa zamani wa klabu ya Mamelod Sundowns Steve Komphela kuchukua nafasi ya Kocha Abdelhack Benchika aliyeondoka klabuni hapo kwa makubaliano ya pande mbili baada ya kudumu kwa muda mfupi.

Kocha huyo mwenye miaka 56 ya kuzaliwa kwa sasa anaifundisha klabu ya Lamontiville Golden Arrows Fc inayoshiriki ligi kuu ya soka nchini Afrika ya kusini ambayo imemaliza ligi kuu nchini humo ikiwa katika nafasi ya tisa ya msimamo ambapo Mamelod Sundowns wameibuka mabingwa.

Kocha huyo ana uzoefu wa kutosha akiwa amewahi kutumika kama kocha msaidizi katika klabu za Kaizer Chiefs na Mamelod Sundowns kwa nyakati tofauti tofauti.

banner

Mazungumzo baina ya mabosi wa klabu ya Simba sc na kocha huyo yanaendelea kwa njia ya mtandao na endapo atafikia muafaka basi anaweza kujiunga na klabu hiyo yenye nia ya kurejesha ufalme wake uliopotea kwa muda mrefu nchini.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited