Site icon Sports Leo

Mtibwa Wakubali 5g ya Simba sc

Baada ya kuambulia kipigo cha mabao 5-0 timu ya Mtibwa Sugar imekubali kuwa ilizidiwa kimchezo na wekundu hao wa Msimbazi.

Simba iliifunga Mtibwa mabao hayo matano huku ikicheza kwa kiwango kikubwa sana huku wakitoa burudani kwa mashabiki wake.

Kocha wa Mtibwa Sugar alikiri kuzidiwa kimbinu na Simba sc huku akitaja kuwa wachezaji wake 8 walikua kwenye mfungo wa mwezi wa Ramadhani hivyo kuzidiwa kwa kikosi chake kilikua kitu alichokitarajia.

Mabao ya Simba sc yalifungwa na Meddie Kagere,Rally Bwallya na Cletous Chama.

Exit mobile version