Home Makala Mwalimu Achukua Tuzo Septemba

Mwalimu Achukua Tuzo Septemba

by Sports Leo
0 comments

Mshambuliaji wa klabu ya Fountain Gate Fc Selemani Mwalimu Gomez amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa mwezi Septemba kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Bodi ya Ligi kuu nchini (Tplb).

Mshambuliaji huyo ambaye kwa sasa yupo katika kambi ya timu ya Taifa inayojiandaa na mchezo wa marudiano dhidi ya Dr Congo,amechaguliwa baada ya kucheza jumla
Dakika 353 kwa mwezi Septemba na kufanikiwa kufunga jumla ya Magoli 3 katika mwezi huo.

Selemani Mwalimu kawashinda William Edgar (Fountain Gate) na Feisal Salum (Azam FC) ambapo pia mpaka sasa ndie anaongoza katika orodha ya wafungaji bora wa ligi kuu akiwa na mabao saba.

Mwalimu ambaye amesajiliwa akitokea ligi kuu ya Zanzibar amekua na mwanzo mzuri ambapo akiwa na mwendelezo huu anaweza kutwaa kiatu cha ufungaji bora ambacho kinamilikiwa na Stephan Aziz Ki wa Yanga sc aliyefunga mabao 21 msimu uliopita.

banner

Kutokana na kiwango chake kocha Hemed Morocco amemjumuisha mchezaji huyo katika kikosi cha timu ya Taifa kwa mara ya kwanza japo hakucheza mchezo dhidi ya Congo ugenini Stars ulipochapwa 1-0.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited