Home Makala Mwamnyeto Ajifunga Yanga sc

Mwamnyeto Ajifunga Yanga sc

by Sports Leo
0 comments

Beki mahiri na nahodha wa klabu ya Yanga sc Bakari Nondo Mwamnyeto amesaini kandarasi mpya ya miaka miwili kuendelea kusalia katika klabu ya Yanga sc baada ya ule wa awali kufikia tamati mwishoni mwa msimu huu.

Nahodha mwenyeji wa mkoa wa Tanga sc alijiunga na Yanga sc akitokea Coastal union miaka miwili iliyopita na mwezi wa saba alikua anamaliza mkataba wake wa awali ambao uliigharimu klabu ya Yanga sc zaidi ya milioni 200 ikiwemo dau la usajili la staa huyo pamoja na gharama ya kuvunja mkataba wake ambao Yanga sc ililipa milioni 150 kwa Coastal union pamoja na kuwapa udhamini wa jezi.

Beki huyo tangu ajiunge na Yanga sc amekua na kiwango bora kabisa huku pia akipata nafasi katika timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa stars’ ambapo pia licha ya klabu yake ya Yanga sc pia Simba sc na Azam fc zilikua zinamvizia kumsajili kitasa huyo.

banner

Yanga sc ipo katika mkakati wa kuwaongezea mikataba mastaa wake ambao mikataba yao imeisha wakianza na Kibwana Shomari na sasa ni Mwamnyeto huku wengine mazungumzo yakiwa yanaendelea.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited