Klabu ya Kaizer chiefs imeonyesha ya kumhitaji mlimzi wa kushoto na nahodha anayemaliza mkataba ndani ya klabu ya Simba Sc Mohammed Hussein Zimbwe ambaye yuko mbioni kumaliza mkataba wake mwishoni mwa msimu huu 2024-2025.
Hii inakuwa ni mara ya pili Kwa klabu hiyo kuhitaji huduma yake baada ya kufanya hivyo misimu miwili nyuma licha kuendelea kumkosa kutokana na Simba Sc kushinda Vita hizo za usajili.
Mkataba wa Simba Sc na Mohamed Hussein unaelekea ukingoni na walishaketi mara mbili bila mafanikio yoyote kwa pande zote mbili ambapo suala kubwa likiwa na maslahi.
Uongozi wa Simba umejipanga kurejea tena mezani na mlinzi huyo baada ya kukamilika kwa mchezo wa fainali wa kombe la shirikisho barani Afrika dhidi ya klabu ya Rs Berkane.
Hata hivyo kuna asilimia kubwa kwa klabu hiyo kumkosa tena kutokana na wachezaji wengi hasa waliojihakikishia nafasi katika klabu walizopo kutotaka kuhama kirahisi rahisi.