Site icon Sports Leo

Ndayiragije Atemwa Stars

Taarifa za awali zinadai kuwa shirikisho la soka nchini Tanzania lipo mbioni kumtema kocha wa timu hiyo Ettiene Ndayiragije baada ya kuwa na mfululizo wa matokeo yasiyoridhisha hasa katika michuano ya Chan 2021 nchini Cameroon.

Ingawa bado shirikisho hilo halijathibitisha taarifa hizo lakini tayari lipo mbioni kumuajiri aliyekuwa kocha wa zamani wa timu hiyo Kim Poulsen huku likificha kuwa anaajiri kwa nafasi ipi katika kocha wa vijana ama timu kubwa.

Wadau wengi wa soka hapa nchini wamekua wakikosoa mbinu za Ettiene aliyewahi kuzifundisha timu za Mbao Fc na Azam Fc hasa katika uchaguzi wa kikosi ambapo hivi karibuni aliwatema baadhi ya mastaa na kuita wachezaji wachanga katika kikosi cha Chan.

Exit mobile version