Nyota wa Chelsea Callum Hudson-Odoi ameamua kuchagua kuiwakilisha timu ya Taifa Ghana badala ya England ambayo alichagua kuiwakilisha awali kutokana na kufanyiwa vitendo vya kibaguzi.
Cullum mtoto wa nyota wa zamani wa klabu ya heart Oak ya Ghana Bismark Odoi amefikia uamuzi huo baada ya kutofurahishwa na vitendo vya ubaguzi walivyofanyiwa wachezaji watatu wa England wenye asili ya Africa Marcus Rashford, Bukayo Sacka na Jordan Sancho baada ya kukosa mikwaju ya penati kwenye mchezo wa fainali dhidi ya Italy.
lakini pia inaelezwa jambo lingine lililomvutia nyota huyo ambaye alizaliwa England kuichagua timu ya Taifa ya Ghana ni upendo alionyeshwa na raia wa Ghana pamoja na Rais wa nchi hiyo Akufo Ado alipotembelea Ikulu ya nchi