Site icon Sports Leo

Nyota Mpya Yanga sc Matatani

Fiston Abdoulrazack mshambuliaji mpya wa mabingwa wa kihistoria nchini Yanga SC ameingia mzozo na wakala wake wanaofahamika kama HERITAGE SOCER AGENCY kwa madai kwamba amekiuka mkataba na kusaini Yanga bila ridhaa yao kama wasimamizi.

Katika barua yao ambayo wameiandika kwa Yanga SC na kuinakili kwa FIFA, CAF na TFF HERITAGE wanadai kukiukwa na mchezaji pamoja na mawakala wengine wa Kitanzania ambao waliwatumia katika kumtafutia nafasi.

Kampuni hiyo imedai mchezaji huyo waliwasiliana nae wiki hiyo hiyo na hakusema kama amepata dili la klabu hiyo lakini wanashangaa kusikia kuwa tayari amesaini mkataba na wanajangwani hao.

Exit mobile version