Home Makala Ofa Zamiminika Kwa Zimbwe

Ofa Zamiminika Kwa Zimbwe

by Sports Leo
0 comments

Beki wa klabu ya Simba Sc Mohammed Hussein Zimbwe amepata ofa kadhaa kutoka klabu za nje ya Tanzania ambazo zimeonyesha nia ya kumsajili wakati wa dirisha kubwa la usajili mwishoni mwa msimu huu.

Dili hizo zimebainishwa na Meneja wa mchezaji huyo Carlos Mastermind ambaye amesema kuwa mpaka sasa bado hawajakaa kujadili kuhusu ofa hizo na punde watakapokaa watafanya uamuzi sahihi.

“Kuna klabu ya Afrika Kusini imetualika kufanya mazungumzo.Kuna klabu ya Libya imeonyesha kumtaka. Kama uongozi wa mchezaji hatujakaa naye kujua mpango wake ni upi lakini tutakaa”,Alisema meneja huyo ambaye pia anamsimamia mchezaji Kibu Dennis.

banner

Hata hivyo pamoja na dili hizo bado ni ngumu kwa beki huyo kuondoka katika klabu ya Simba Sc kutokana na umuhimu wake kikosini humo licha ya kwamba mkataba wake unaelekea ukingoni.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited