Aliyekuwa kiungo mshambuliaji wa klabu ya Simba sc Agustine Okrah amejiunga na klabu ya Bechem United ya Ghana baada ya kuachana na klabu hiyo kwa makubaliano ya pande zote mbili baada ya kutumika kwa msimu mmoja pekee
Kwa mujibu wa taarifa kutoka katika Moja ya jarida kubwa la Michezo la nchini Ghana jarida hilo limeripoti kuwa kiungo huyo ameingia makubaliano ya kusaini mkataba wa mwaka mmoja tu na waliokuwa Waajiri wake hao,
Mara baada ya kutambulishwa Kwa mashabiki nyota huyo amekabidhiwa jezi namba 10 alivyokuwa akiivaa kabla hajasajiliwa Simba sc.
” Okrah rasmi amerejea katika klabu yake ya zamani ya Bechem aliyokuwa anaichezea kabla ya kujiunga na Simba katika msimu uliopita”,
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Okrah alikua mchezaji muhimu klabuni hapo kabla hajajiunga na Simba sc ambapo majeraha yalikua kikwazo kwake kutimiza malengo yake.