Home Makala Onyango Akubali Yaishe

Onyango Akubali Yaishe

by Sports Leo
0 comments

Beki kisiki wa klabu ya Simba sc Joash Onyango amekubali kuungana na kambi ya klabu hiyo baada ya kamati ya sheria na hadhi za wachezaji nchini kukataa ombi lake la kuvunja mkataba na klabu ya hiyo kutokana na kutotimizwa kwa baadhi ya makubaliano katika mkataba wake.

Awali Onyango alisaini mkataba wa miaka miwili kusalia klabuni hapo lakini kukatokea sintofahama iliyochagizwa na kuwasili kwa beki Mohamed Outtara ambaye alimuweka benchi beki huyo staa wa timu ya taifa ya Kenya huku kocha Zoran Maki akipendelea zaidi pacha mpya ya Outtara na Inonga na kumuacha Onyango benchi.

Pamoja na beki huyo kugoma kujiunga na kambi ya klabu hiyo pia alishinikiza kuvunja mkataba wa mwaka mmoja uliobaki klabuni hapo ili akatafute malisho mengine ambapo aliwasilisha maombi ya kuvunja mkataba huo kwa kamati hiyo ambayo iligoma kupitisha ombi hilo na kumuamuru arudi kambini kuungana na timu kitu ambacho tayari ametekeleza na ameungana na msafara wa timu kuelekea jijini Mbeya ambapo wataivaa Prisons kesho Jumatano.

banner

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited