Klabu ya Orlando Pirates ya Afrika Kusini imehamia kwa kocha wa klabu ya Simba Sc Fadlu Davis Baada ya kuambiwa kuwa José Luis Riveiro hatokuwa sehemu ya benchi la ufundi kuelekea msimu ujao.
Fadlu aliwahi kuifundisha klabu hiyo kama kocha msaidizi na sasa klabu hiyo imefanya jitihada za kumrudisha ambazo mpaka sasa zimegonga mwamba baada ya kocha huyo kugomea dili hilo.
Mbali na klabu hiyo pia klabu ya Raja Club Athletic kutoka Morocco na wao walifika mezani kwa Fadlu Davids lakini mtaalamu huyo akawajibu kuwa hayupo tayari kwa sasa.
“Sipo tayari kuondoka kwa sasa na natamani nifanikiwe zaidi nikiwa hapa Simba Sc” Alisema kocha huyo baada ya kuulizwa kuhusu ofa hizo zilizofika mezani kwake.
Fadlu amevivutia vilabu hivyo kutokana na kuifanya Simba sc kuwa tishio ndani ya muda mfupi tangu ajiunge nayo akichukua nafasi ya Roberto Oliveira “Robertinho” aliyetimuliwa klabuni hapo baada ya kufungwa 5-1 na Yanga sc.