Home Makala Pamba Jiji Fc Yamvuta Bwalya

Pamba Jiji Fc Yamvuta Bwalya

by Sports Leo
0 comments

Kiungo mshambuliaji wa zamani wa klabu ya Simba Sc Rally Bwalya yupo mbioni kukamilisha dili ya kujiunga na klabu ya Pamba Jijini Fc ya jijini Mwanza kwa mkataba mfupi wa miezi sita.

Mabosi wa Pamba Jiji Fcwl wanapambana kukamilisha dili hilo mapema na tayari wapo nchini Zambia wakimalizana na mabosi wa Napsa Stars ya nchini humo anayoichezea mchezaji huyo kwa sasa.

Pamba jiji Fc baada ya kutofanya vizuri katika duru la kwanza la ligi kuu ya Nbc wakizoa alama 12 pekee wakiwa katika nafasi ya 13 ya msimamo wa ligi kuu ambapo sasa wameamua kusajili vifaa vya maana wakiwemo Deus Kaseke,Hamad Majimengi na Habib Kyombo ambao baadhi wamewapata kws mkopo na dili la Bwalya linakuja kuongeza nguvu zaidi.

banner

Bwalya mchezaji wa zamani wa Simba sc kabla ya kutumkia Afrika ya kusini alikokaa kwa muda na kisha kurejea nchini Zambia ana uwezo wa kucheza vizuri zaidi nafasi ya kiungo mshambuliaji namba 10,8 pamoja na winga zote mbili.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited