Klabu ya Simba sc imekutana na figisu za kuwatoa mchezo kuelekea mchezo wao wa klabu bingwa barani Afrika dhidi ya Plateau United ya nchini Nigeria.
Katika kufanikisha azma ya kuwatoa mchezoni vijana hao wa msimbazi klabu hiyo ilipanga kuwasingizia kuwa na Virusi vya Corona mastaa wa klabu ya Simba sc akiwemo Cletous Chama na Jonas Mkude huku pia wakigomea mechi hiyo kuonyeshwa mubashara kupitia Azam Tv.
Mtendaji mkuu wa klabu ya Simba sc Barbara Gonzalez amesema kupitia mtandao wa Instagaram ”
“Plateau United wamekataa kuruhusu mechi kurushwa mubashara. Licha ya juhudi zetu zote tukishirikiana na mshiriki wetu AZAM TV, mwenyeji wetu amekataa kushirikiana kwenye hilo.
“Nichukue nafasi hii kuomba radhi kwa wapenzi wetu wote ulimwenguni ambao walitaka kuangalia mechi hii. Mpaka muda huu, tunapigania hii mechi iweze kuoneshwa mubashara (live).” Alisema Ceo huyo wa kwanza mwanamke wa klabu hiyo.