Site icon Sports Leo

Pyramids Fc Yakomaa na Mayele

Klabu ya soka ya Pyramid Fc ya nchini Misri imeendelea kumshawishi mshambuliaji Fiston Mayele kusaini mkataba mpya ili kuendelea kusalia klabuni hapo baada ya kuridhishwa na kiwango chake msimu huu.

Kwa mujibu wa mwanahabari Kutoka nchini Misri, Khaled El Ghandour, klabu hiyo imewasilisha ofa mpya ya mkataba kwa wawakilishi wa Fiston Mayele ambayo inaripotiwa kuwa na thamani ya kati ya R55 milioni hadi R74 milioni kwa msimu ambayo ni sawa na takriban shilingi za kitanzania bilioni 7.2 hadi bilioni 9.7 kwa mwaka kulingana na viwango vya sasa vya ubadilishaji wa fedha.

Licha ya ofa hii kubwa, El Ghandour anadai kuwa kuna uwezekano mkubwa Fiston Mayele akaondoka klabuni hapo baada ya fainali ya Kombe la Misri itakayochezwa usiku huu saa 2:30 usiku kwa saa za Tanzania.

Mustakabali wa Fiston Mayele umeendelea kuwa gumzo kubwa, huku vilabu kama Kaizer Chiefs na Al Ahly vikihusishwa kwa Ukaribu na mshambuliaji huyo wa raia wa Congo DRC.

Ofa hii nono kutoka Pyramids FC inaonesha nia yao ya kutaka kumbakisha, lakini hatma yake bado haijulikani kama ataongeza mkataba ama ataendelea na msimamo wake wa kuhitaji kuondoka klabuni hapo.

Exit mobile version