Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan leo amezungumzia suala la ubovu wa viwanja vya soka nchini huku akikitaka chama cha mapinduzi(Ccm) kukarabati viwanja ambavyo wanavimiliki ama wawakaribishe wawekezaji waviendeshe viwanja hivyo.
Rais huyo wa kwanza mwanamke nchini Alisema hayo wakati anahutubia vijana wa jiji la Mwanza katika mkutano maalumu ambapo ulitoa fursa kwa vijana kuongea na Rais huyo kuelezea changamoto mbalimbali katika mkutano uliofanyika katika uwanja wa Nyamagana katikakati ya jiji.
“Viwanja vingi vya Michezo vinamilikiwa na Chama cha Mapinduzi nakiomba chama kikarabati viwanja hivyo na Kama wanashindwa basi watafute wawekezaji ili viwanja viwekwe nyasi za bandia kwani michezo ni ajira”Alisema Rais Samia
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
