Klabu ya Aston Villa imethibitisha kukamilisha usajili wa mshambuliaji Marcus Rashford raia wa England kwa mkopo mpaka mwishoni mwa msimu huu 2024-2025 akitokea Manchester United.
Aston Villa italipa asilimia 75 ya mshahara wa Rashford hadi mwezi Juni mwaka huu huku kukiwa na kipengele cha kumnunua jumla kwa ada ya pauni milioni 40.

Rashford (27) ambaye alijiunga na Mashetani hao Wekundu akiwa na umri wa miaka saba anaondoka klabuni hapo baada ya miaka 20 akiwa amepachika magoli 138 kwenye michezo 426.
“Nimefurahi sana kutua kwenye kikosi cha Aston Villa. Nilikuwa na bahati ya timu nyingi kunitaka, lakini Villa lilikuwa chaguo langu rahisi sana, napenda jinsi wanavyocheza msimu huu, nifuraha kuwa hapa na nasubiri kwa hamu kubwa siku ya kuingia uwanjani,” alisema Rashford wakati anatambulishwa.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Hata hivyo, inaelezwa kuwa mshambuliaji huyo ambaye ameitumikia timu ya Taifa ya England mechi 60 anatarajiwa kuendelea kupokea kitita chake kilekile cha mshahara cha pauni 350,000 kwa wiki na mkataba wake na United unatarajiwa kumalizika Juni 2028.
