Home Makala Robertinho Kutimka Rayon Sc

Robertinho Kutimka Rayon Sc

by Sports Leo
0 comments

Aliyewahi kuwa kocha wa klabu ya Simba Sc Roberto Oliveira (Robertinho) ambaye hivi majuzi alisimamishwa kazi na Rayon Sports kwa sababu za kimatibabu, amewasilisha malalamiko kwa Chama cha soka cha Rwanda (FERWAFA) akitaka kulipwa Dola za Kimarekani 20,000 ambayo ni mshahara wa miezi minne.

Kocha huyo aliugua na kulazimika kusimamishwa kazi ili akaweke afya yake imara kabla ya kurejea kwenye majukumu yake klabuni hapo jambo linaloonekana kuwa gumu kwa sasa.

Kocha huyo tayari ameiandikia barua FERWAFA akiomba kulipwa mishahara ya miezi minne sawa na Dola 20,000 na ndani ya wiki tatu ili kuachana salama na klabu hiyo kabla ya kupeleka mashitaka yake shirikisho la soka Duniani (FIFA).

banner

Robertinho (64), ambaye analipwa Dola 5,000 kwa mwezi, hivi majuzi aliiomba Rayon Sports kumlipa deni lake na kurejea nyumbani kwao Brazil kwa sababu hana la kufanya Kigali.

Kocha huyo alikuwa amesimamishwa siku 30 na Rayon Sports ikiwa na maana kuwa msimu kwake ulikuwa umemalizika tayari klabuni hapo.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited