Home Makala Ronaldo Aimaliza Ghana

Ronaldo Aimaliza Ghana

by Sports Leo
0 comments

Mshambuliaji wa timu ya Taifa ya Ureno Cristiano Ronaldo amechangia kiasi kikubwa kwa ghana kupoteza mchezo wa kwanza katika fainali za kombe la dunia zinazoendelea nchini Qatar akiisaidia Ureno kuibuka na alama tatu kwa ushindi wa mabao 3-2.

Ronaldo ndie aliyefunga bao la kwanza kwa penati baada ya kuangushwa na beki  Mohammed Salisu dakika ya 65 na kumfanya kuwa mchezaji wa kwanza kufunga bao katika michuano mitano ya kombe la dunia ambapodakika ya 73 Andrew Ayew alisawazisha bao hilo lakini dakika tano mbele Ureno waklifunga bao la pili lililofungwa na Joao Felix akipokea pasi ya Bruno Fernandes na dakika ya 80 Rafael Leao akifunga bao la tatu.

Ghana walifanikiwa kupata bao la pili na mwisho katika mabao matano ya mchezo huo likifungwa na Osamane Bakari dakika ya 89 ya mchezo huo.

banner

Ureno sasa imepanda mpaka kileleni mwa kundi H ambapo sare baina ya Ubelgiji na Korea Kusini imewafanya wagawane alama.

Pamoja na kufunga bao hilo la uongozi Ronaldo hakumaliza dakika 90 za mchezo huo ambapo alifanyiwa mabadiliko dakika za mwisho ambapo mashabiki walimpigia makofi na kumshangilia licha ya kutokua na klabu baada ya Manchester United kuamua kuvunja mkataba wake kwa makubaliano ya pande mbili.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited