Home Makala Ronaldo Atambulishwa Rasmi Uarabuni

Ronaldo Atambulishwa Rasmi Uarabuni

by Sports Leo
0 comments

Staa wa zamani wa klabu ya Real Madrid na Manchester United Cristiano Ronaldo ametambulishwa rasmi kama mchezaji mpya wa klabu ya Al-Nassr inayoshiriki ligi kuu nchini Saudi Arabia baada ya kuwasili nchini humo mapema siku ya juzi baada ya kuvunja mkataba wake na klabu ya Manchester united kwa makubaliano ya pande mbili.

Ronaldo mapema baada ya fainali za kombe la dunia ambapo timu yake ya Taifa ya Ureno ilitolewa na Morroco katika hatua ya robo fainali alisaini mkataba wa miaka miwili na klabu ya Al-Nassr ambapo atakua akilipwa kuliko mchezaji mpira wa miguu yeyote yule duniani.

Zaidi ya mashabiki 25000 walijaa katika uwanja wa raucous Mrsool Park mjini Riyadh kumshudia staa huyo akitambulishwa ambapo alisema kuwa “Najisikia fahari kwa uamuzi huu mkubwa katika maisha yangu,Barani ulaya kazi yangu imeisha na nimeshinda kila kitu na sasa ni muda wa changamoto mpya”.

banner

“Nashukuru Al Nassr wamenipa nafasi hii si tu kwa ajili ya mpira bali kwa ajili ya kizazi kijacho na kizazi cha wanawake,Kwangu hii ni changamoto lakini najisikia furaha na najivunia sana”.

“Nilikua na fursa  nyingi ulaya,Brazil,Australia na Marekana hata Ureno klabu nyingi zilitamani kunisajili lakini niliamkua kuja hapa na hii ni nafasi nzuri ya kukuza alama muhimu hapa kwa uzoefu na ujuzi wangu”.

Inaripotiwa kwamba katika mkataba huo wa miaka miwili Ronaldo atalipwa kiasi cha paundi 160 milioni kwa mwaka ambapo ndiye mwanasoka anayelipwa zaidi kwa sasa.

 

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited