Jonas Mkude ambaye ni winga wa Simba ameeleza sababu kubwa iliyomfanya ashindwe kujiunga na timu ya Taifa ‘Taifa Stars’ ni matatizo ya kibinadamu yanayomkabili na siyo suala la utovu wa nidhamu.
Nyota huyo alichelewa kujiunga na timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars iliyokuwa imeweka kambi kwa ajili ya kujiwinda na michuano ya CHAN iliyotarajiwa kufanyika nchini Cameroon kabla haijaahirishwa kutokana na maambukizi ya virusi vya Coronavilivyoingia duniani.
“Haina maana kwamba mimi ni mtovu wa nidhamu ndio maana nilichelewa kujiunga na timu ya Taifa hapana ninaithamini kazi yangu lakini masuala ya kibinadamu ndiyo ambayo yamekuwa yakinitatiza na kushindwa kuwahi kwenye kambi”alisema Mkude
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.