Home Soka Samia Aruhusu Kuiona Stars Vs Algeria Bure

Samia Aruhusu Kuiona Stars Vs Algeria Bure

by Sports Leo
0 comments

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dk Samia Suluhu Hassan amenunua tiketi zote za mchezo baina ya Timu ya Taifa ya Tanzania dhidi ya Guinea wa kuwania kufuzu michuano ya mataifa ya Afrika mwaka 2025 nchini Morocco.

Rais Samia amenunua tiketi hizo ili kutoa fursa kwa mashabiki kuingia bure ikiwa ni moja ya mkakati wa kuongeza hamasa katika mchezo huo utakaofanyika siku ya Jumanne Novemba 19 katika uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam ambapo Stars ikishinda basi itakua imekata tiketi moja kwa moja kushiriki michuano hiyo mikubwa barani Afrika.

Katika msimamo wa kundi H Congo Dr imefuzu ikiwa na alama 12 huku Guinea ikiwa nafasi ya pili ya msimamo na alama 9 na Taifa Stars ipo nafasi ya tatu na alama 7 huku Ethiopia ikiwa na alama 1 mkiani ambapo endapo Stars ikishinda basi moja kwa moja itafuzu katika kundi hilo kama mshindi wa pili lakini ikipata sare ama kufungwa basi haitofuzu.

banner

Tayari Kocha wa Taifa Stars Hemed Morocco amewaijumuisha mastaa wazoefu kama Mbwana Samata na Saimon Msuva ambao walikua chachu ya ushindi dhidi ya Ethiopia ugenini nchini Congo Dr.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited