Home Makala Sereri Aizamisha Simba Sc

Sereri Aizamisha Simba Sc

by Sports Leo
0 comments

Mshambuliaji mpya wa klabu ya Azam Fc Zidane Sereri ameikosesha alama tatu klabu ya Simba Sc baada ya kusawazisha bao dakika za lala salama katika mchezo wa ligi kuu ya Nbc nchini baina ya Simba Sc na Azam Fc uliomalizika kwa sare ya 2-2.

Mchezo huo uliofanyika katika uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam majira ya saa moja jioni ulishuhudia bao la mapema kwa Azam Fc likifungwa na Gibril Sillah dakika ya kwanza ya mchezo baada ya kupokea pasi ya Idd Nado.

banner

Azam Fc walitumia vyema makosa ya Fabrice Ngoma na kupata bao hilo huku wakikosa umakini zaidi kwani walikua na mtego mzuri wa kushambulia kwa kushtukiza.

Simba sc ilivyokua ikiwategemea mastaa Ellie Mpanzu na Kibu Dennis sambamba na Lionel Ateba ambapo Kibu Dennis alimpasia pasi nzuri Mpanzu aliyewazidi maarifa mabeki na kipa wa Azam Fc na kusawazisha bao hilo dakika ya 25.

Mpaka mapumziko timu hizo zilikua sare lakini kipindi cha pili Simba sc walipunguza kasi na kuufanya mchezo uwe wa kushambuliana zamu kwa zamu.

Abdulrazak Hamza alifunga bao la pili kwa kichwa na kuipa Simba sc uongozi akimalizia kazi ya Jean Charles Ahoua dakika ya 76 ya mchezo huo.

Wengi wakiwa wamekata tamaa na kuamini Simba sc itachukua alama tatu lakini kocha Rachid Taoussi aliamua kumuingiza Zidane Sereri dakika ya 82 ya mchezo ambapo dakika ya 88 alipokea pasi ndefu ya Feisal Salum na kumzidi maarifa kipa Moussa Camara na kufunga bao la kusawazisha na kufanya mpira kumalizika kwa sare ya 2-2.

Simba sc sasa imefikisha alama 51 ikiwa na michezo 20 katika nafasi ya pili ya msimamo wa ligi kuu ya Nbc nchini huku Azam Fc ikisalia katika nafasi yake ya tatu na alama 44.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited