Kiungo mshambuliaji wa klabu ya Yanga sc Stephane Aziz Ki ameiongoza klabu hiyo kuifunga Timu ya Stand United kwa mabao 8-1 katika mchezo wa robo fainali ya kombe la Shirikisho la Crdb nchini.
Mchezo huo uliofanyika katika uwanja wa Kmc Complex uliopo Mwenge jijini Dar es Salaam umeshuhudia kiungo huyo akihusika katika mabao sita kati ya nane ambapo alifunga manne na kutoa asisti mbili na kupata tuzo ya mchezaji bora wa mchezo huo.
Stand United ni kama walitaka kushindana na Yanga sc kwa kucheza bila nidhamu ya ulinzi na kujikuta wakipata kipigo hicho kikubwa.
Aziz Ki alifunga bao la kwanza dakika ya 16 ya mchezo kisha Nickson Kibabage kufunga bao la pili dakika ya 20 huku Chama akifunga mabao mawili ya haraka dakika ya 32 na 40 ya mchezo.
Kipindi cha pili Stand United pia waliruhusu mabao manne mengine kupitia kwa Azizi Ki dakika za 51,60 na 64 kisha Kennedy Musonda aliyeingia kuchukua nafasi ya Prince Dube alifunga bao la nane dakika ya 86 ya mchezo huo.
Yanga sc sasa baada ya ushindi huo itavaana na Jkt Tanzania katika mchezo wa nusu fainali huku endapo itafuzu kwenda fainali ya itakutana na mshindi kati ya Simba sc dhidi Stand United.
Â