Home Soka Simba Sc Kukipiga na Al Hilal Fc

Simba Sc Kukipiga na Al Hilal Fc

by Sports Leo
0 comments

Klabu ya Simba Sc inatarajiwa kucheza mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Klabu ya Al Hilal Fc ya nchini Sudan utakaofanyika jijini Dar es Salaam katika uwanja wa Kmc Complex tarehe 31 August.

Kocha Fadlu Davis anatarajiwa kuutumia mchezo huo kukiweka imara kikosi chake kabla ya kuvaana na Al Ahly Tripoli ya Libya katika mchezo wa raundi ya pili ya michuano ya kombe la Klabu bingwa barani Afrika katikati ya mwezi Septemba.

Baada ya mchezo huo wa kirafiki mastaa watatu wa klabu ya Simba sc wanatarajiwa kujiunga na kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) ambapo kipa Ally Salim,Mohammed Hussein na Edwin Balua wataungana na mastaa wengine kuunda kikosi cha Taifa Stars dhidi ya Guinea na Ethiopia kuwania tiketi ya kufuzu Afcon 2025.

banner

Pia mastaa wengine kama Moses Mukwala,Valentino Nouma na Mousa Camara nao wataungana na timu zao za Taifa kwa ajili ya michezo hiyo ya kimataifa ya kuwania kufuzu Afcon 2025.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited