Klabu ya Simba sc imeshusha viingilio vya eneo la mzunguko katika mchezo wa kombe la shirikisho hatua ya makundi dhidi ya Asec Mimosa kutoka shilingi elfu tano mpaka elfu tatu tu.
Hayo yamesemwa na tajiri wa klabu hiyo bilionea Mohamed Dewji ili kuongeza chachu ya mashabiki kujaa uwanjani zaidi kuishangilia klabu hiyo inapokwenda kuanza safari ya kuwania kuchukua taji hilo ambalo miaka ya themanini walifanikiwa kuingia fainali lakini wakapoteza mchezo huo.
Simba sc itakua na kibarua kizito ikicheza takribani michezo mitatu ya hatuan ya makundi ndani ya siku 14 huku iktakiwa kusafiri ugenini mara moja kuwavaa USGN ya nchini Algeria.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Simba sc imeingia katika hatua ya makundi ya kombe la shirikisho baada ya kuitoa Red Arrows ya nchini Zambia katika hatua ya mtoano.