Home Makala Simba sc Waisubiri Gendamarie

Simba sc Waisubiri Gendamarie

by Sports Leo
0 comments

Baada ya kushindwa kufuzu dhidi ya Asec Mimosa ya Ivory Coast katika mchezo wa hatua ya makundi ya kombe la shirikisho barani Afrika na kuambulia kipigo cha mabao 3-0 sasa klabu ya Simba sc imeelekeza nguvu katika mchezo wa mwisho dhidi ya Us Gendamarie ya nchini Niger.

Simba sc katika msimamo wa kundi D ina jumla ya alama 7 huku Asec Mimosa wakiwa kileleni mwa kundi na alama 9 wakati Berkane wakiwa na alama 7 huku Us Gendamarie ambao walitoa sare ya 2-2 dhidi ya Rs Berkane wenyewe wakiwa nafasi ya 4 ya msimamo wa kundi hilo.

Ili Simba sc ifuzu michuano hiyo haina budi kuifunga Gendamarie huku akiombe sare ama mmoja apoteze mchezo baina ya Rs Berkane na Asec mimosa.

banner

Kipigo cha mabao 3-0 ilichopata Simba sc kimetoa taswira ya uwezo wa kikosi hicho kupata alama tatu hasa kikiwa ugenini baada ya kushindwa kufurukuta pamoja na kuruhusu mashambulizi ya mara kwa mara huku uwezo wa kipa Aishi Manula ukiwaokoa baada ya kucheza mikwaju miwili ya penati.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited