Site icon Sports Leo

Simba Sc Yaangusha Alama Mtwara

Klabu ya Simba sc imekubali kuambulia alama moja katika mchezo wa ligi kuu nchini dhidi ya Namungo Fc uliofanyika katika uwanja wa Majaliwa ulioko wilaya ya Ruangwa mkoani Mtwara.

Simba sc ikianza na kikosi bila kuwa na mastaa wake Cletous Chama,Henock Inonga na Sadio Kanoute huku pia ikimkosa Shomari Kapombe katika eneo la ulinzi japo eneo la mbele ilikua na mastaa wake Saido Ntibanzokiza na Jean baleke Othos ambaye aliindikia bao timu hiyo dakika ya 28.

Hassani Kabunda alitumia vyema makosa ya kipa Ally Salim ya kuupangua vibaya mpira wa kona ambao ulimkuta mfungaji huyo na kuisawazishia Namungo Fc katika  dakika ya 39 ya mchezo huo bao ambalo lilidumu mpaka dakika 90 za mchezo huo.

Simba sc iliamua kupumzisha baadhi ya mastaa wake kwa ajili ya mchezo wa nusu fainali dhidi ya Azam Fc utakaofanyika Jumapili Mei 7 mkoani Mtwara.

Baada ya matokeo hayo sasa Simba sc imefikisha alama 64 nyuma ya Yanga sc yenye alama 68 ikiwa kileleni na mchezo mmoja mkononi.

Exit mobile version