Site icon Sports Leo

Simba sc Yaleta Mbrazil kuwanoa Kina Manula

Klabu ya Simba imekamilisha usajili wa kocha wa makipa Milton Nienov raia wa Brazil kuchukua nafasi ya Mohamed Mwalami aliyefutwa kazi tangu October 29 mwaka Jana.

Milton ambaye amewahi kuzifundisha timu za Free State, Polikwane na Golden Arrows za Afrika kusini yupo jijini Dar Salaam muda wowote kuanzia sasa atatambulishwa kuwa kocha wa makipa wa klabu ya Simba kwa mkataba wa miaka miwili.

Kocha huyo atakua na jukumu kubwa la kuwanoa makipa Aishi Manula na Beno Kakolanya kuhakikisha wanapambana na mastraika wasumbufu katika hatua ya makundi ya klabu bingwa barani Afrika.

Exit mobile version