Home Soka Simba Sc Yamtambulisha Lawi

Simba Sc Yamtambulisha Lawi

by Sports Leo
0 comments

Klabu ya Simba sc imetambulisha beki Lameck Lawi kama usajili wake wa kwanza msimu huu kutoka Coastal Union ya jijini Tanga baada ya kutoa taarifa za kuachana na wachezaji watano mpaka sasa.

Lawi ametajwa kama usajili wa kwanza wa klabu hiyo ambapo ametambulishwa kupitia mitandao ya kijamii rasmi ya klabu hiyo ambapo taarifa zinasema kuwa usajili huo pamoja na kutambulishwa bado umewagawa mabosi wa Coastal Union.

banner

Mashabiki wengi wa klabu hiyo wanaona usajili wa beki huyo unakuja kuipa nguvu safu ya ulinzi ya timu hiyo hasa akicheza pacha na Che Fondoh Malone huku ikijulikana kuwa Henock Inonga Baka hana tena mpango wa kuendelea kuitumikia timu hiyo.

Beki huyo kijana alikua mhimili mkubwa katika safu ya ulinzi ya Coastal Union kuanzia msimu uliopita ambapo alichukua tuzo ya mchezaji bora chipukizi huku msimu huu akipandisha kiwango chake maradufu kiasi cha kuiwezesha Coastal kufuzu michuano ya kombe la Shirikisho barani Afrika.

Simba sc imetoa utambulisho wa mchezaji huyo bila picha rasmi kinyume na ilivyozoelekea ikitajwa kuwa imewahi kumtambulisha baada ya kugundua kuwa kuna hila kutoka kwa viongozi wa Coastal kughairisha dili hilo baada ya kupata ofa nono zaidi.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited